Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:23

Marekani yatangaza msaada mpya wa dola bilioni moja kwa Ukraine


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (Kushoto0 na mwezake wa Ukraine Dmytro Kuleba wakihutubia waandishi wa habari mjini Kiev, Ukraine. Agosti 6, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (Kushoto0 na mwezake wa Ukraine Dmytro Kuleba wakihutubia waandishi wa habari mjini Kiev, Ukraine. Agosti 6, 2023.

Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani Antony Blinken alitangaza msaada mpya wa zaidi ya dola bilioni 1 kwa Ukraine, wakati wa ziara yake mjini Kyiv Jumatano, ambao alisema utasaidia  Ukraine "kuongeza kasi" ya kukabiliana na Russia, katika vita vinavyoendelea.

Marekani imeipatia Ukraine zaidi ya dola bilioni 40 kama msaada wa kiusalama tangu Russia ilipovamia nchi hiyo mwaka jana, zikiwemo silaha ambazo Kyiv inasema ni muhimu katika kudhibiti vikosi vya Russia.

"Leo, tunatangaza usaidizi mpya wa jumla ya zaidi ya dola bilioni 1 katika juhudi hizi za pamoja," Blinken alisema katika mkutano na waandishi wa habari na mwenzake wa Ukraine Dmytro Kuleba.

"Mssda huu unajumuisha dola milioni 665.5 katika usaidizi mpya wa kijeshi na usalama wa raia," aliongeza waziri Blinken.

Katika hafla nyingine, Blinken alitangaza kwamba Marekani ilikuwa ikifanya kazi na Ukraine kutafuta njia mbadala za usafirishaji wake wa nafaka, baada ya kuvunjika kwa mkataba wa mauzo ya nafaka wa Bahari ya Black Sea mwezi Julai na kuweka meli hatarini. Ukraine, ambayo imekuwa ikiomba msaada zaidi wa nchi za Magharibi, ilianzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya majeshi ya Rusia mwezi Juni, baada ya kuimarisha vikosi vyake, na kupata silaha nyingi kutoka kwa mataifa ya Magharibi.

Forum

XS
SM
MD
LG