Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:49

Marekani yaiondolea Sudan marufuku ya kusafiri


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Serikali ya Marekani imeiondoa Sudan kutoka katika orodha ya nchi sita zenye Waislam walio wengi ambazo zilikuwa zimewekewa katazo la kusafiri kwa raia wake na imeongeza katika orodha hiyo mataifa matatu Venezuela, Chad na Korea Kaskazini.

“Rais wa Marekani Donald Trump Jumapili (Septemba 24) ameiondoa Sudan kutoka katika katazo jipya la kusafiri lililotolewa mwezi Machi uliopita ambalo lilikuwa la kwanza kuwekwa kwa nchi sita zenye Waislam walio wengi,” tovuti yenye ofisi zake Paris ya Sudan Tribune imeripoti.

“Kuondolewa kwa katazo hilo kumetokea wiki mbili kabla ya uamuzi wa kudumu wa kubatilisha vikwazo vya uchumi dhidi ya Sudan ambalo wengi walikuwa wanalitarajia kufanyika Octoba 12,” habari hizo zimeeleza.

Wachambuzi wameeleza kuwa hatua hiyo ni dalili ya kuwa vikwazo vilivyokuwa vimewekwa dhidi ya Sudan vitaondoshwa na ni matunda ya Khartoum kutoa ushirikiano kwa Marekani katika kupambana na ugaidi.

Wasafiri wanaotaka kuja Marekani kutoka nchi nane watakabiliwa na katazo jipya ambalo limerekebisha amri ya katazo la kusafiri la kwanza ambalo tayari limesainiwa na Rais Donald Trump Jumapili.

Amri mpya ambazo zitaanza kutumika Octoba 18, zitawaathiri raia wa Chad, Iran, Libya, Korea Kaskazini, Somalia, Syria, Venezuela na Yemen.

Maafisa wa Marekani wamesema kuwa nchi hizi zimekataa kutoa ushirikiano katika kubadilishana taarifa kuhusu ugaidi na masuala mengine na Marekani.

XS
SM
MD
LG