Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:45

Marekani yadhibitisha kuokolewa kwa msichana wa Yazidi kutoka Gaza


Msichana wa kabila la Yazidi aiyeokolewa kutoka Gaza baada ya utuma wa miaka mingi.
Msichana wa kabila la Yazidi aiyeokolewa kutoka Gaza baada ya utuma wa miaka mingi.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Alhamisi imedhibitishia VOA kuhusu operesheni uliokuwa ngumu ya kuokoa raia wa Iraq na aliyekuwa mtumwa wa ngono kwenye kundi la Islamic State, kutoka Gaza akipitishiwa Israel.

Kutokana na mizozo ya kidiplomasia ya muda mrefu kati ya Israel na Iraq, ilichukua miezi kadhaa ya juhudi za wanaharakati wa haki za binadamu, pamoja na ujumbe wa kidiplomasia wa Marekani wa kieneo, kupanga operesheni ya kuokoa mwanamke huyo. Ushirikiano kati ya Israel, Jordan, Iraq na Umoja wa Mataifa ulitumika kuikamilisha.

Oktoba mosi mwaka huu, Marekani ilisaidia katika kumuondoa kwa njia salama msichana huyo wa Kiyazidi kutoka Gaza, hadi kuunganishwa na familia yake nchini Iraq, kulingana na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani akizungumza na VOA. Fawzia Amin Saydo mwenye umri wa miaka 21 alitekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State kutoka mji wake wa nyumbani wa Sinjar, Agosti 2014, akiwa amebakisha mwezi mmoja kufikisha umri wa miaka 11.

Yeye na ndugu zake wawili wenye umri wa miaka 7 na 10 walikuwa miongoni mwa maelfu ya watu kutoka kabila la Yazidi, waliotekwa nyara na Islamic State, kutokana na Imani yao ya kidini. Ingawa ndugu zake baadaye waliweza kutoroka, Saydo alibaki wakati akipitia manyanyaso pamoja na ubakaji kutoka wa wanamgambo wa ISIS. Mapema 2015, alipelekwa kwenye mji wa Syria wa Raqqa ambapo alifungwa jela, na kubakwa kabla ya kuozeshwa kwa lazima kwa mpiganaji wa ISIS kutoka Palestina aliyekuwa na umri wa miaka 24 wakati huo.

Forum

XS
SM
MD
LG