Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:41

Matumaini ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Sudan yazidi kufifia


Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan

Matarajio ya makubaliano ya kusitisha mapigano kutokana na mazungumzo ya amani nchini Sudan yaliyofadhiliwa na Marekani wiki hii hayapo mezani kwa sasa, kwani pande zinazopigana hazijathibitisha kuhudhuria kwao.

“Tumekuwa na mawasiliano ya awali na RSF. Tumekuwa na mawasiliano ya kina na jeshi la Sudan( SAF). Lakini bado hawajatupa uthibitisho, ambao ungekuwa muhimu leo ili kusonga mbele Agosti 14,”, Tom Perriello, mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya Sudan, aliwambia waandishi wa habari mjini Geneva Jumatatu.

Perrielo alisema “Tutasonga mbele na washirika wetu wa kimataifa kufikia mpango wa utekelezaji, mpango wa utekelezaji madhubuti kuhusu jinsi gani tunaweza kusonga mbele hadi kukomesha ghasia na kupata usambazaji kamili wa misaada ya kibinadamu, na utaratibu wa ufuatiliaji wa utekelezaji. Mambo haya yalikuwa yafanyike muda mrefu uliopita.”

Umoja wa Mataifa unauchukulia mzozo wa Sudan kama mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu duniani. Mzozo huo mbaya ambao umeikumba Sudan umesababisha zaidi ya watu milioni 10.7 kuwa wakimbizi wa ndani ya nchi na kuwalazimisha wengine milioni 2 kukimbilia nchini jirani kutafuta hifadhi.

Forum

XS
SM
MD
LG