Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 19:22

Marekani kuimarisha kamandi yake ya kijeshi nchini Japan


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken na waziri wa mambo ya kigeni wa Japan Yoko Kamikawa, wakiwa kwenye mkutano wa G7 mjini Tokyo .Nov. 8, 2023.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken na waziri wa mambo ya kigeni wa Japan Yoko Kamikawa, wakiwa kwenye mkutano wa G7 mjini Tokyo .Nov. 8, 2023.

Marekani Jumapili imetangaza hatua mpya madhubuti ya kuimarisha kamandi yake ya kijeshi nchini Japan, ili kuongeza ushirikiano na vikosi vya Japan, wakati mataifa yote mawili yakikubaliana kuwa China ndiyo changamoto kubwa zaidi ya kimkakati, inayokumba eneo hilo.

Tangazo hilo ni kufuatia mazungumzo ya kiusalama kati ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken na mwenzake wa Ulinzi Lloyd Austin, na wenzao wa Japan Yoko Kamikawa na Minoru Kihara. Baada ya mazungumzo hayo, Austin ameambia wanahabari kwamba Marekani itaimarisha vikosi vyake vilivyoko Japan, kwa kuunganisha makao makuu, pamoja na kupanua operesheni zake.

Taarifa ya pamoja kutoka kwa mawaziri hao imesema kuwa mfumo mpya wa kamandi utatekelezwa sambamba na mpango wa Tokyo wa kubuni kamandi ya pamoja ya vikosi vyake kufikia Machi mwaka ujao. Taarifa hiyo pia imekashifu kile kimetajwa kuwa tabia ya kichokozi ya Beijing, kwenye bahari ya Kusini na Mashariki mwa China, ambako inafanya mazoezi ya kijeshi na Russia, pamoja na kupanua utengenezaji wa silaha za nyuklia.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa sera za kigeni za Beijing zinazingatia kubadili mfumo wa kimataifa ili kujinufaisha wenyewe, huku wakiumiza wengine.

Forum

XS
SM
MD
LG