Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 12:03

Ufilipino na Japan zaingia makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi


Ufilipino na Japan zitatia saini makubaliano ya ulinzi leo Jumatatu ambayo yataruhusu vikosi vyao vya kijeshi kutembelea ardhi za kila nchi hizo, ofisi ya mawasiliano ya rais wa Ufilipino imesema Jumapili.

Rais Ferdinand Marcos Jr atashuhudia utiwaji saini wa makubaliano ya ufikiwaji wao kati ya Ufilipino na Japan muda mfupi baada ya wito wa heshima wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Yoko Kamikawa na Waziri wa Ulinzi, Minoru Kihara, ofisi yake imesema.

Kamikawa na Kihara wako Manila kukutana na wenzao wa Ufilipino Jumatatu ili kujadiliana kuhusu kuimarisha ushirikiano katika ulinzi kati ya washirika wawili wakuu wa Marekani barani Asia.

Ufilipino imekuwa ikiimarisha uhusiano na majirani zake na nchi zingine ili kukabiliana na kile inachoelezea kuwa uvamizi wa China unaokua katika Bahari ya Southern China.

Forum

XS
SM
MD
LG