Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:59

Marekani kufungua ubalozi mdogo Sahara ya magharibi


 Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Mike Pompeo amesema Ijumaa Washington imeanza utaratibu wa kufungua ubalozi mdogo katika Sahara ya magharibi.

Hatua hii imechukuliwa na serikali ya Marekani ikiwa ni wiki chache tu baada ya utawala wa Trump kutambua rasmi madai ya Morocco ya kumiliki koloni hilo la zamani la hispania.

Wanawake wa Sahrawi wakitembea katika kambi ya wakimbizi ya Al Smara iliyoko jangwani huko Tindouf, kusini mwa Algeria, Machi 4, 2016.
Wanawake wa Sahrawi wakitembea katika kambi ya wakimbizi ya Al Smara iliyoko jangwani huko Tindouf, kusini mwa Algeria, Machi 4, 2016.

Koloni hilo linalogombaniwa na chama cha ukombozi cha Sahrawi.

Taarifa ya Pompeo inaeleza kwamba ubalozi huo mdogo ambao hautakuwa na mtu huko utasimamiwa na ubalozi wa Marekani nchini Morocco.

XS
SM
MD
LG