Akiongea katika bustani ya Rose Garden akiwa pamoja na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, Trump ameahidi “kuchukua hatua madhubuti” dhidi ya programu ya nyuklia na makombora ya Pyongyang.
“Hizi sio zama za kuvuta subira juu ya serikali ya Korea Kusini ambayo imefeli kutekeleza wajibu wake,” amesema Trump, akionyesha utaratibu wa wale viongozi waliomtangulia katika kukabiliana na mgogoro wa Korea Kaskazini ulivyofeli. "Imechukua miaka mingi na imeshindikana, na kwa kweli, hakuna kuvuta subira hivi sasa."
Trump na Moon walitofautiana jinsi ambavyo wanatakiwa waweke shinikizo juu ya Korea Kaskazini ili iweze kuacha kabisa programu yake ya nyuklia. Viongozi wote wawili pia wamekosoa baadhi ya maeneo ya ushirikiano wa nchi zao katika ulinzi.
Lakini ilikuwa wazi kwamba nchi hizo mbili siku ya Ijumaa zilionyesha mshikamano wao na msimamo wao wa pamoja.