Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:08

Sharti la kuingia Marekani kwa nchi sita ni udugu au biashara


Maelekezo kwa wasafiri wa kimataifa wanaowasili uwanja wa ndege wa Seattle-Tacoma International Airport, Juni 26, 2017, Seattle, Washington.
Maelekezo kwa wasafiri wa kimataifa wanaowasili uwanja wa ndege wa Seattle-Tacoma International Airport, Juni 26, 2017, Seattle, Washington.

Marekani itaanza Alhamisi kutekeleza kanuni mpya zinazowataka watu wanaoomba viza kutoka nchi sita zenye Waislam wengi, lazima wawe na ndugu wa karibu au biashara nchini Marekani.

Shirika la Associated Press limesema kuwa kanuni hizo mpya zitaanza kutumika saa 8 p.m muda wa Washington Alhamisi (0000GMT), na wasafiri kutoka nchi hizo watatakiwa kukidhi vigezo hivyo vipya vya kuingia nchini.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje iliowafikia mashirika ya habari ya Associated Press na Reuters, Jumatano, jioni sana, lakini haikutolewa kwa umma, imeainisha jinsi maafisa wa ofisi za visa za ubalozi wanavyotakiwa kuendelea kushughulikia maombi ya viza kutoka kwa raia wa Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen.

Undugu wa karibu unaokubaliwa ni pamoja na mzazi, mke, mume, watoto, mtoto mkubwa (wa kike na kiume), shemeji, au ndugu wa damu ambaye tayari yuko Marekani.

Mahusiano ambayo hayakidhi kigezo hiki ni bibi au babu, mjukuu, baba (mkubwa au mdogo), mama (mkubwa au mdogo), mpwa, ndugu kwa upande wa baba (mkubwa au mdogo) au mama (mkubwa au mdogo), shemeji, mchumba au wanafamilia wengine.

Mahusiano ya kibiashara yanayoruhusiwa ni lazima yawe “rasmi kwenye nyaraka” na hayakutengenezwa kwa ajili ya kukwepa katazo la kusafiri. Tamko hilo limesema kitu kama vile kuomba nafasi katika hoteli ya kufikia haiwezi kukidhi kigezo hicho cha kuingia Marekani.

XS
SM
MD
LG