Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 03:12

Marekani: Benki ya First Republic yafungwa, mali zake kuuzwa kwa Benki ya JPMorgan Chase


FILE PHOTO: Mlinzi akiwa analinda nje ya Tawi la Benki ya First Republic huko San Francisco,California, April 28, 2023.
FILE PHOTO: Mlinzi akiwa analinda nje ya Tawi la Benki ya First Republic huko San Francisco,California, April 28, 2023.

Mdhibiti wa Marekani alisema Jumatatu wameifunga benki ya First Republic na kufikia makubaliano ya kuuza mali zake  kwa benki ya JPMorgan Chase. Benki ya First Republic ina jumla ya mali zinazofikiwa dola bilioni 229.1 hadi kufikia  April 13.

Hiyo ni benki kubwa ya tatu ya Marekani kushindwa kuendesha shughuli zake katika miezi miwili.

Benki ya JP Morgan ni moja ya wanunuzi kadhaa waliokuwa na shauku ya kununua mali hizo ikiwemo kampuni za PNC Financial Services Group, na Citizens Financial Group Inc, ambazo ziliwasilisha zabuni ya mwisho Jumapili katika mnada unaoendeshwa na wadhibiti wa Marekani, vyanzo vinavyofahamu suala hilo vilisema mwishoni mwa wiki.

Makubaliano ya First Republic, ambayo ina mali zenye thamani ya dola bilioni 229.1 kufikia Aprili 13, yamekuja chini ya miezi miwili baada ya benki za Silicon Valley na Signature kushindwa kuendesha shughuli zake katikati ya wakopeshaji wa Marekani kuondosha fedha zao, na kuilazimisha Benki Kuu ya Marekani kuingilia kati na kuchukua hatua za dharura kuimarisha masoko. Kushindwa huko kulitokea baada ya sarafu ya crypto –iliyolenga benki ya Silvergate kujiondoa katika soko kwa uamuzi wake.

XS
SM
MD
LG