Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:25

Aliyechoma moto misikiti Minneapolis akamatwa


Polisi wa Minneapolis wamemkamata mwanamme anayeshukiwa kuwasha mioto miwili ambayo iliharibu misikiti katika jiji hilo wiki iliyopita kama sehemu ya kile mkuu wa polisi alichokiita jaribio la kuleta vitisho  katika jamii ya Kiislamu.

Mkuu wa polisi Brian O'Hara alitangaza kukamatwa kwa Jackie Rahm Little mwenye umri wa miaka 36 mapema Jumapili lakini hakutoa maelezo ya jinsi alivyokamatwa.

Anashtakiwa kwa kushiriki kuchoma moto hapo Aprili 23 na 24 na hati ya kukamatwa ilitolewa.

Mkuu huyo wa polisi katika taarifa yake ya Jumapili amesema kuchoma moto jengo takatifu, ambako familia na watoto hukusanyika, ni unyama mkubwa sana, na hawatavumilia kiwango hicho cha chuki ya wazi katika jiji la Minneapolis.

Viongozi walio katika baraza la Mahusiano ya Kislamu na Marekani wa Minnesota walipongeza kukamatwa kwa mtu huyo baada ya tukio la moto ambalo halikuwatia hofu jamii ya Waislamu katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG