Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 02:23

Tamasha la vijana linaloungwa mkono na USAID linafanyika Ethiopia


Ramani ya Ethiopia ikijumuisha mikoa yake pamoja na nchi zilizo jirani nae
Ramani ya Ethiopia ikijumuisha mikoa yake pamoja na nchi zilizo jirani nae

Tamasha hilo chini ya kaulimbiu “Be Inspired, Own Your Future” linafanyika karibu miezi sita baada ya makubaliano ya amani kutiwa saini ili kumaliza vita vya miaka miwili na wakati serikali ya Ethiopia ikiwa imeanza mazungumzo na kundi la waasi la Oromo Liberation Army (OLA)

Tamasha la vijana linalofadhiliwa na Marekani lilifunguliwa mwishoni mwa wiki nchini Ethiopia kauli mbiu ikiwa ni “Be Inspired, Own Your Future”. Tamasha hilo la siku mbili limefanyika miezi michache tu baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili kumalizika katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia na wakati ambapo mazungumzo ya amani yameanza na waasi wa Oromo Liberation Army.

Tamasha la vijana linaloungwa mkono na USAID lilianza Jumamosi nchini Ethiopia, ambapo takriban vijana 20,000 kutoka kote nchini humo walishiriki.

Tamasha hilo, chini ya kaulimbiu, “Be Inspired, Own Your Future”, linafanyika karibu miezi sita baada ya makubaliano ya amani kutiwa saini ili kumaliza vita vya miaka miwili na wakati serikali ya Ethiopia ikiwa imeanza mazungumzo na kundi la waasi la Oromo Liberation Army (OLA).

Balozi wa Marekani nchini Ethiopia Tracey Ann Jacobson alizungumzia umuhimu wa tamasha hilo katika hotuba yake ya ufunguzi.

Lengo ni kutoa fursa za ajira, fursa za mikopo, kutoa fursa nzuri kwa uongozi na huduma za afya kwa vijana kote Ethiopia, nimeona fursa ikikua kutoka kwenye mbegu ndogo ambayo tuliipanda mwezi Machi hadi kuwa mpango huu wa kushangaza ambao tunaushuhudia leo

Waziri wa Wanawake na Masuala ya Jamii wa Ethiopia, Ergoge Tesfaye alizungumza katika hafla hiyo kuhusu kushughulikia udhaifu kwa vijana.

Taasisi za serikali na zisizo za kiserikali, wanajamii wengine, pamoja na vijana wenyewe, wanatakiwa kuelewa kuwa wanakabiliwa na matatizo mbalimbali pamoja na uwezo huu ambao haujaguswa na kutoa suluhish na pia hatua muhimu zinazotarajiwa kutoka kwetu sote.

Wiki iliyopita, serikali ya Ethiopia ilianza mazungumzo na wawakilishi wa OLA nchini Tanzania baada ya miaka mingi ya mzozo wa muda mrefu wa kikabila katika mkoa wa Oromia nchini Ethiopia.

Wajasiriamali na watu wenye ubunifu kutoka miji 17 nchini Ethiopia wanaonyesha kazi zao katika tamasha la Addis Ababa, lakini tukio hilo halikuwa na wawakilishi kutoka mkoa wa Tigray kwa sababu ya athari za vita.

Boni Bekele, kutoka mkoa wa Oromia, ana kibanda cha nguo katika maonyesho ya soko la ndani katika tamasha hilo. Anasema kwamba alikuwa na uwezo wa kufanya kazi nchi nzima katika miaka ya nyuma lakini sio tena kwa wakati huu.

Serikali imewafanya mamilioni ya vijana kupoteza matumaini. Nguvu zao zinapaswa kutumiwa, na siyo kutumikatu kama wanajeshi, kwa sababu hilo halitaibadilisha nchi. Ni falsafa, sayansi na ujuzi unaoweza kuibadilisha nchi. Lazima hili lipewe kipaumbele.

Tamasha la vijana pia liliangazia kijiji cha teknolojia na nyumba ya sanaa.

Mmoja wa wasanii waliowasilisha kazi yake ni Melat Shiferaw mwenye umri wa miaka 23, ambaye alitokea Dire Dawa mashariki mwa Ethiopia.

Kwake yeye, hata hivyo, mazingira ya sasa katika nchi si ya kutia moyo, ana matumaini mambo haraka yatarudi kuwa kawaida hivi karibuni.

Kama binadamu, hatuishi tu kufikiria kuhusu leo, bali kile tunachotarajia kesho. Kwa hivyo, licha ya hali yoyote tunayopitia sasa hivi, si mazingira ya kufanya kazi, sisi bado tuna matumaini ya kesho na tunafanya kazi kwa bidii kwa hilo, kwa sababu mtu anatarajia kesho itakuwa bora zaidi.

Tamasha hilo linaloungwa mkono na USAID kwa miaka mitano, linatarajiwa kujumuisha washiriki kutoka Tigray katika miaka ijayo, wakati waandaaji wakikamilisha tathmini ya baada ya mzozo wa kisiasa katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG