Waziri Mkuu wa muda wa taifa hilo la Afrika Magharibi Kanali Abdoulaye Maiga alihalalisha hatua hiyo katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, na kuitaja kuwa ni jibu kwa Ufaransa kusitisha misaada ya maendeleo kwa Mali hivi karibuni.
Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilisema wiki iliyopita ilifanya uamuzi huo, ambao ulikuja miezi mitatu baada ya kukamilisha mchakato wa kuviondoa vikosi vyake, vya kupambana na wapiganaji wa Kiislamu, kutoka nchi hiyo, juu ya madai ya Bamako ya kutumia wanamgambo wa kundi la Wagner la Russia.
Wiki iliyopita, chanzo cha wizara ya mambo ya nje kilisema Ufaransa itadumisha misaada yake ya kibinadamu pamoja na kufadhili "mashirika ya kiraia" nchini Mali.