Kwa mujibu wa barua ambayo imeonwa na shirika la habari la Reuters, unakuwa ni mshangao mwingine mpya wa mataifa kadhaa ya Afrika magharibi kujiondoa katika taifa hilo kwa mwaka huu.
Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba kujiondoa huko kumethibitishwa na vyanzo viwili vya ngazi ya juu vya usalama.
MINUSMA ambayo ndiyo tume ya kulinda amani ya Mali, na serekali ya Mali pamoja na Ivory Coast yenyewe hazikujibu haraka uwepo wa taarifa hizi.
Moja ya mataifa ya nchi ambayo yana ghasia, Mali kwa muongo mmoja imekuwa ikitegemea washirika wa kikanda na walinda Amani kuwakabili wanamgambo wenye msimamo mkali ambao wameshaua maelfu ya watu na kuchukuwa maeneo makubwa ya katikati na kaskazini mwa nchi.