Wachambuzi ambao baadhi walihudhuria vikao hivyo wanasema kwamba ziara hiyo ilikuwa mfano wa namna Hsiao anavyokusudia kutangamana na wengine mara baada ya kuapishwa mwezi Mei akiwa na rais mteule Lai Ching-te. Wakati wa ziara yake, kiongozi huyo alikutana na viongozi wa bunge kwenye Jamhuri ya Czech, Poland na Lithuania.
Pia alikutana na zaidi ya wabunge 30 kutoka bunge la Ulaya mjini Brussels, akiwemo naibu spika wa bunge la Ulaya Othmar Karas. Kulingana na wizara ya mambo ya kigeni ya Taiwan, Hsiao amesisitiza uhusiano wa kidenokrasia kti ya Taipei na mataifa ya Ulaya
Forum