Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:47

Tillerson: Mahusiano kati ya Marekani na Russia ‘yalegalega’


Rex Tillerson-Sergei Lavrov
Rex Tillerson-Sergei Lavrov

Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson amesema mahusiano kati ya Marekani-Russia “yalegalega sana,” akionyesha kutokuwepo kwa kuaminiana kati ya nchi hizi mbili.

Maoni hayo aliyatoa Jumatano baada ya masaa kadhaa ya mvutano katika mazungumzo yake huko Moscow na Rais Vladimir Putin wa Russia na Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov.

Putin, akizungumza wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha Russia, alikiri kuwa mahusiano kati ya Washington na Moscow yanalegalega mwaka huu.

Mvutano wa hivi karibuni kati ya Moscow na Washington unahusisha kuchunguza vipi shambulizi la silaha za kemikali lilitokea Syria April 4. Tillerson amesema kuwa Marekani ilikuwa “inauhakika” kuwa “ulipangwa na kusimamiwa na kutekelezwa na majeshi ya serikali ya Syria.

Lakini Lavrov hakutoa maelezo yoyote kuhusu madai ya Russia kwamba shambulizi la gesi ya sarin inaweza kuwa ni kutokana na uchokozi wa wapinzani wa Syria au ulisababishwa na ndege za kivita za Syria zilipopiga dipoti ya silaha ya waasi ambayo inahifadhi gesi ya sarin.

Uchunguzi wa Kina

“Tumesisitiza kuwa kuwepo na uchunguzi wa kina,” Lavrov amesema katika mkutano wa waandishi wa habari alioufanya akiwa na Tillerson. “Tunataka uchunguzi wenye ukweliufanyike.”

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Russia amesema Moscow haiwezi “kumtetea mtu yoyote” aliyehusika na mashambulizi.

Ziara ya Tillerson Moscow imewasilisha mazungumzo ya ngazi ya juu kabisa kati ya Marekani na Russia tangia Trump achukue madaraka Januari.

Mataifa hayo mawili yenye nguvu za nyuklia kuliko nchi zote duniani yamehitalifiana juu ya mambo kadhaa, likiwemo suala la Moscow kuendelea kuwapa msaada waasi wa mashariki ya Ukraine wanaopigana na serikali ya Kyiv, na suala la jumuiya ya kipelelezi ya Marekani iliyokuwa imetangaza kuwa udukuzi uliofanywa na majasusi waliotumwa na Kremlin ulivuruga uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka jana.

Putin na Tillerson, ambaye alikuwa mkuu wa kampuni kubwa ya mafuta ExxonMobil, wanajuana vizuri. Rais wa Russia aliwahi kumpa mkuu huyo wa zamani Nishani ya Kremlin Ya Urafiki, lakini hivi sasa hali ya uhusiano huo imefifia kuliko ilivyokuwa mwanzoni.

Tillerson amesema Jumatano kuwa kitendo cha Russia kuvuruga uchaguzi wa Marekani kilikuwa ni tatizo kubwa ambalo lilikuwa “limekwisha julikana vizuri kabisa.”

Lavrov alipinga hilo na kusema Russia ilikuwa inatolewa kafara juu ya “tuhuma hizo nzito,” na kuongeza : “Lazima niseme tena… hakuna mtu aliyekuja na ushahidi wowote juu ya hili.”

“Tupeni ushahidi” wa uvunjaji sheria wa Russia unaotuhusisha na kuvuruga siasa za Marekani, Lavrov alisema, “na sisi tutajibu.

‘Uwezekano’ wa kuboresha mahusiano

Mashambulizi ya makombora yaliofanywa na Marekani katika kituo cha ndege cha kijeshi nchini Syria wiki iliopita ziliongeza mvutano katika mgogoro wa Syria, ambao hivi sasa uko katika mwaka wake wa saba, Lavrov amesema. Lakini, aliongeza kuwa anaamini kuwa Moscow na Washington wanauwezo mkubwa wa kuboresha mahusiano yao.

XS
SM
MD
LG