Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:16

Mzaliwa wa Kenya ashinda kiti cha Seneti Australia


Lucy Gichuhi, ambaye ni mzaliwa wa Kenya, ameshinda kiti cha useneta nchini Australia.
Lucy Gichuhi, ambaye ni mzaliwa wa Kenya, ameshinda kiti cha useneta nchini Australia.

Mwanamke mzaliwa wa Kenya ameshinda kiti cha useneta nchini Australia baada ya mahakama kuu ya nchi hiyo kuamuru kwamba kura za uchaguzi uliofanyika mwaka jana zihesabiwe tena.

Lucy Gichuhi, sasa anasubiri mahakama kuthibitisha uchaguzi huo.

Iwapo uchaguzi wake utathibitishwa, Gichuhi atakuwa mtu wa kwanza mwenye asili ya kiafrika, kuketi kwenye baraza la bunge la seneti ya nchi hiyo, hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la Australia Broadcasting Corporation (ABC).

Gichuhi aliwania kiti hicho kwa tikiti ya chama cha Family First Party manao July mwaka jana lakini mpinzani wake wa pekee, Bob Day, akakumbwa na kashfa na ikabidi mahakama kuamuru kura hizo zihesabiwe tena.

Akionekana mwenye furaha, Gichuhi ambaye ni wakili anayehudumu nchini Australia, alisema haya baada ya kura kuhesabiwa tena: "Ninashukuru kwa heshima kubwa kwa kupewa nafasi hii ya kuwatumikia wa-Australia....ninalichukulia kama fursa kubwa ya kulitumikia taifa hili kubwa."

Bi Gichuhi, ambaye uraia wake pacha umezua utata, alihamia Australia poamoja na famila yake mnamo mwaka 1999 na kuwa raia wa Australia miaka mitatui baadaye.

Hata hivyo, balozi wa Kenya nchini Australia Isaiya Kabira amenukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema kuwa ubalozi hauna rekodi zinazomuonmyesha mwanasiasa huyo akiomba uraia wa nchi mbili.

-Imeandikwa na BMJ Muriithi, VOA.

XS
SM
MD
LG