Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, chama cha mawakili nchini, LSK, pamoja na shirika la kutetea haki za binadamu la Kenya Human Rights Commission, KHRC, wameiambia mahakama Jumatatu, kwamba Kenya inaweza kujipatia dola bilioni 1.85, zinazohitajika kukarabati uwanja huo jijini Nairobi, bila msaada kutoka nje.
Mashirika hayo yameiambia mahakama kwamba hatua hiyo ni yenye gharama kubwa, inatishia ajira za watu na wala haina faida yoyote kwa walipa kodi wa Kenya, kulingana na nyaraka zilizowasilishwa na KHRC. Kampuni ya Andani haijasema lolote kufuatia hatua hiyo, wakati msemaji wa idara ya kitaifa ya usafiri wa anga, aliiambia Reuters kwamba hawana maoni yoyote kwa kuwa suala hilo liko mahakamani.
Mwezi uliopita, muungano wa wafanyakazi kwenye uwanja huo ulitishia kuitisha mgomo kwa madai kwamba mkataba huo ungepelekea kupoteza ajira kwa wafanyakazi wa Kenya.
Forum