Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 18:03

Mahakama ya Juu Marekani yaidhinisha kutolewa kwa hati za kodi za Trump


TRUMP-IMPUESTOS
TRUMP-IMPUESTOS

Mahakama ya Juu ya Marekani  Jumanne iliidhinisha kutolewa kwa nyaraka za kodi za rais wa zamani Donald Trump, kwa kamati ya Baraza la Wawakilishi, hatua ambayo inaashiria kushindwa kwa mwanasiasa huyo wa chama cha Republican.

Trump alilitaja ombi la jopo hilo, linaloongozwa na wabunge wa chama cha Democratik kuwa ni limechochewa kisiasa.

Majaji hao walikataa ombi la dharura la Trump la Oktoba 31, la kuzuia uamuzi wa mahakama ya chini ilioridhia ombi la Kamati hiyo, kutaka kuziona hati za kodi za mfanyabiashara huyo aliyegeuka mwanasiasa, Hakuna jaji aliyepinga uamuzi huo hadharani.

Kamati hiyo, ambayo imetafuta miaka sita ya rekodi za kodi za Trump, kuanzia mwaka wa 2015 hadi 2020, itakuwa na muda mfupi wa kukamilisha kazi yake kuhusiana kabla ya chama cha Republican kuchukua udhibiti wa baraza la wawakilishi.

Warepublican walipata kura chache kufuatia uchaguzi wa katikati ya muhula wa Nov. 8, na watachukua udhibiti wa Bunge - na kamati - mnamo Januari. Msemaji wa Trump hakujibu mara moja ombi la maoni. Trump alikuwa rais wa kwanza katika kipindi cha miongo minne kutotoa hati zake za kodi huku akitaka kuweka siri habari za utajiri wake na shughuli za kampuni yake ya Trump Organization.

XS
SM
MD
LG