Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 17:50

Mahakama Kuu yasitisha matumizi ya kanuni za mitandao


TCRA
TCRA

Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara nchini Tanzania leo imetoa zuio la muda la amri ya mahakama linalozuia matumizi ya kanuni za maudhui ya kimtandao 2018, ambazo matumizi yake yalipaswa kuanza rasmi Mei 5.

Mahakama hiyo imetoa zuio hilo baada ya taasisi sita kuwasilisha mahakamani maombi ya kuzuia matumizi ya Kanuni hizo April 30, mwaka huu. Kesi ya msingi imepangwa kusikilizwa tarehe 10 may 2018.

Taasisi zilizowasilisha maombi hayo mahakamani ni Kituo cha Sheria na Haki za binadamu ( LHRC), Kituo cha Watetezi wa Haki za Binadamu (THRD), Baraza la Habari la Tanzania (MCT), Jamii Media, Jumuiya ya Waandishi wa Habari WanawakeTanzania (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri Tanzania Editors (TEF).

Taasisi hizi katika kesi ya msingi ya mapatio ya kanuni hizo (judicial review) zimefunguwa mashtaka dhidi ya Waziri wa Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Tanzania katika maombi ya msingi taasisi hizo zinaiomba Mahakama Kuu kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa kigezo kwamba; waziri ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake ( Ultra vires), Zinakiuka kanuni za usawa (natural justice), Kanuni hizo zinapingana na haki ya kujieleza, haki ya kusikilizwa, na haki ya usiri.

XS
SM
MD
LG