Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 20:16

Mahakama Kuu Malawi yabatilisha ushindi wa Rais Mutharika wa 2019


Rais Peter Mutharika
Rais Peter Mutharika

Mahakama ya kikatiba nchini Malawi Jumatatu imefutilia mbali uchaguzi uliompa ushindi Rais Peter Mutharika mwezi Mei 2019, na kuagiza uchaguzi kurudiwa tena.

Mahakama imetoa uamuzi huu baada ya kujiridhisha na vielezo vya vyama vya upinzani juu ya mapungufu mbalimbali yaliyo kuwepo katika uchaguzi huo, Shirika la Habari la Reuters linaripoti.

Mutharika, rais wa Malawi tangu mwaka 2014, alishinda uchaguzi kwa kupata kura asilimia 38.57 na kiongozi wa chama cha upinzani Lazarus Chakwera alipata asilimia 35.41 na Makamu wa Rais Saulos Chilima, aliyeunda chama chake alipata asilimia 20.24 katika hisabu ya mwisho ya majumuisho ya kura.

Tume ya uchaguzi ilimtangaza Mutharika kuwa mshindi katika kinyang’anyiro hicho pamoja na kuwepo malalamiko juu ya mapungufu mengi ikiwemo makaratasi ya matokeo yakiwa na baadhi ya vifungu vilivyofutika au kubadilishwa kwa kufutwa kwa wino maalum.

Mutharika alikuwa ameahidi kupambana na ufisadi na kufufua uchumi katika kipindi chake cha pili cha miaka mitano.

Lakini Chakwera, mpinzani mkuu wa rais, na Chilima walikataa matokeo na kufungua kesi Mahakama Kuu wakitaka matokeo hayo yabatilishwe.

Katika uamuzi wa pamoja, jopo la majaji watano liliamuru kuwa uchaguzi mpya wa rais ufanyika katika kipindi cha siku 150.

XS
SM
MD
LG