Rais amehoji hayo Jumatatu, Ikulu jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kuwaapisha mawaziri wawili na makamishna wa Jeshi la Polisi.
“Tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, baada ya tukio hilo tukamuona Mambosasa (Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa), anakunywa chai na aliyetekwa, baadaye tukaonyeshwa nyumba inayodaiwa kuwa alivyotekwa alihifadhiwa humo.
“Huyo mwenye nyumba alikuwa mtuhumiwa wa kwanza tulitegemea afikishwe mahakamani, kimya mpaka leo miezi imepita sasa hiyo inatoa maswali mengi ambayo majibu hayapo.
“Labda ndiyo mambo ya kisasa kama lilivyo kamanda Mambosasa wa hapa Dar es Salaam… kwa sababu Watanzania walitaka kujua huyo mwenye nyumba ni nani na angekuwa wa kwanza kukamatwa… Hata kama Watanzania watanyamaza lakini mioyo yao haitakuwa kimya,” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amesema anashangaa kwani wanaodaiwa kumteka walimtupa katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, wakaacha silaha zao huku wakijaribu kuchoma gari moto lakini ilishindikana.
“Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania si wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo linaacha maswali….
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.