Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:36

Rais Magufuli amteua Profesa Juma kuwa Jaji Mkuu Tanzania


Jaji Mkuu wa Tanzania
Jaji Mkuu wa Tanzania

Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli amemteua Profesa Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, uteuzi huo unaanza Jumapili ( Septemba 10, 2017).

Kabla ya Uteuzi huo Profesa Ibrahim Hamis Juma alikuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania ambapo alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman.

Taarifa hiyo ya Ikulu inasema Profesa Ibrahim Hamis Juma ataapishwa kesho Septemba 10, 2017 saa nne asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

XS
SM
MD
LG