Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:13

Maelfu ya raia wa Cameroon kuandamana wiki hii


Mpinzani wa rais Paul Biya akiwainulia ngumi polisi wakati wa maandamano huko Paris, tarehe 22 2020. Picha na AFP.
Mpinzani wa rais Paul Biya akiwainulia ngumi polisi wakati wa maandamano huko Paris, tarehe 22 2020. Picha na AFP.

Nchini Cameroon, maelfu ya watu wanaandamana wiki hii, wakitoa wito wa amani na maridhiano kabla ya Siku ya Kitaifa Mei 20.

Misafara ya amani inayoongozwa na wanaharakati, viongozi wa dini na watawala wa kijadi wanaotaka kukomeshwa kwa matamshi ya chuki na mzozo wa kujitenga ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya 6,000 nchini humo tangu mwaka 2017.

Kundi la vijana linaongoza mamia ya raia wa Cameroon katika maandamano yanayopinga matamshi ya chuki katika mji mkuu, Yaounde, siku ya Alhamisi. Waandamanaji hao pia wametoa wito wa kuwepo kwa amani na maridhiano katika taifa hilo la Afrika ya kati.

Waandaaji wanasema maandamano hayo yalianza katika miji na vijiji vyote nchini Cameroon siku ya Jumatatu kabla ya Siku ya Kitaifa Mei 20.

Maelfu ya Wakristo kutoka makanisa ya kikatoliki, Presbyterian na Baptist ya Cameroon walijiunga na maandamano hayo mjini Yaounde siku ya Alhamisi.

Mkurugenzi wa mawasiliano katika Baraza la Kitaifa la Maaskofu nchini Cameroon, mchungaji Humphrey Tatah Mbui alisema Wakristo hawawezi wakawa hawajali wakati kuna ongezeko la matamshi ya chuki na kauli za kuwachukia wageni zinasababisha migogoro na kuharibu taswira ya Cameroon.

Mbui alisema mapigano kati ya jamii yaliongezeka nchini Cameroon baada ya uchaguzi wa rais mwaka 2018 uliokuwa na utata ambapo Rais Paul Biya alitangazwa mshindi. Kiongozi wa upinzani Maurice Kamto pia alijitangazia ushindi huo.

Kwa kuongezea, baadhi ya jamii zinazozungumza Kifaransa zimekuwa zikiwashutumu wale wanaozungumza Kiingereza waliohama kutokana na mzozo wa kujitenga huko Magharibi kuwa wapiganaji au wafuasi.

XS
SM
MD
LG