Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 09, 2025 Local time: 21:05

Maandamano Misri yaongezeka nguvu


Wanasheria Misri wakiwa katika maandamano kwenye uwanja wa Tahrir Square, February 10, 2011
Wanasheria Misri wakiwa katika maandamano kwenye uwanja wa Tahrir Square, February 10, 2011

Maelfu ya madaktari na wanafunzi wa udaktari Misri wanasema wanajiunga na maandamano dhidi ya serikali leo, ikiwa ni sehemu ya nguvu mpya iliyosababisha serikali kuchukua hatua mpya ya ulinzi katika majengo ya serikali, pamoja na makazi ya rais.

Ongezeko la idadi ya waandamanaji na uwepo wa wanajeshi katika mitaa ya Cairo kunaleta wasiwasi kuhusu mpaka lini jeshi litakuwa na msimamo wa kutounga mkono upande wowote katika mgogoro huo.

Maelfu wa wafanyakazi kote nchini Misri wanafanya migomo kwa siku ya pili kupinga mishahara midogo na hali mbaya za ufanyaji kazi. Makundi mapya, wengi wao wakiwa wafanyakazi wenye ujuzi mkubwa, yanajounga na maandamano hayo ambayo yameingia siku ya 17 tangu yaanze.

Waandamanaji wanaendelea kukusanyika nje ya jengo la bunge, ikiwa ni hatua ya kujaribu kupanua upinzani wao nje ya uwanja wa Tahrir. Vifaru zaidi viliwekwa Alhamisi katika barabara inayoelekea makazi ya rais. Waandamanaji wamesema tena na tena wanapanga kuandamana hadi makazi ya rais kudai Rais Hosni Mubarak ajiuzulu.

XS
SM
MD
LG