Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 28, 2024 Local time: 20:37

Jeshi la Misri lawasihi raia kuacha migomo


Polisi wakiandamana mjini Cairo wakidai malipo bora, 14 Februari 2011
Polisi wakiandamana mjini Cairo wakidai malipo bora, 14 Februari 2011

Utawala mpya wa kijeshi nchini Misri umesihi kumalizwa kwa mlolongo wa migomo ambayo inafanyika nchi nzima baada ya mapinduzi,huku wakiashiria nia ya kutaka kushirikiana madaraka na raia na kurekebisha katiba kwa kutumia kura ya maoni.

Baraza kuu la kijeshi linalotawala limetoa taarifa fupi Jumatatu kuwasihi viongozi wa wafanyakazi kumaliza migomo, likionya kwamba migomo hiyo inatishia harakati zozote za kufufua uchumi wa nchi ulioathiriwa vibaya na wiki mbili za maandamano ya upinzani.

Lakini jeshi hilo limesita kupiga marufuku migomo, huku likijaribu kuwahakikishia viongozi wa upinzani kwamba wana nia ya dhati kwa mabadiliko ya kidemokrasia.

Miongoni mwa makundi maarufu yaliyoshiriki mgomo kamili ama sehemu ya migomo hiyo yanayotokea kote nchini Misri ni pamoja na maofisa polisi, wafanyakazi wa viwanda vya nguo, wafanyakazi wa saruji, waajiriwa wa benki za umma na manispaa, wafanyakazi wa sekta za mafuta na gesi, na madereva wa mabasi. Wafanyakazi hao wameelezea masikitiko yao, ikiwemo pia haja ya malipo mazuri na usalama kazini.

XS
SM
MD
LG