Waandishi wa habari wameandamana nje ya makao makuu ya jeshi kwenye mji wa mpakani wa Tijuana, ambapo Rais Andre Manuel Lopez Obrador alifanya mkutano wake wa kila siku na waandishi wa habari, jana alhamisi.
Hali ya mvutano kati ya waandishi wa habari na serikali ya Obrador, inaonekana kuongezeka kila siku.
Hii ni baada ya kuuawa kwa waandishi wa habari watano, wawili kati yao katika mji wa Tijuana, katika wiki sita za kwanza za mwaka 2022, huku rais akiendelea kuwakosoa waandishi wa habari.
Waandishi hao walibeba picha na kusoma majina ya karibu waandishi wenzao 50 ambao wameuawa nchini Mexico tangu mwaka 2018 na kutaka uchunguzi kamili na wa kina kufanyika kuhusiana na vifo vyao.