Kundi hilo la wahamiaji, wakiwemo raia kutoka nchi nane, walianza safari jumamosi kutoka mji wa kusini wa Tapachula, wakisema kwamba wanatka haki, uhuru na maslahi yao kutiliwa maanani.
Wahamiaji hao wamesafiri kwa mguu kwenye barabara kuu kutoka jimbo la Chiapas, kwa uangalizi wa maafisa wa usalama na ulinzi wa wahamiaji
Wana matumaini ya kuingia Marekani.
Wamekuwa Tapachula kwa mda wa miezi miwili ambapo maafisa wa uhamiaji na tume ya uhamiaji ya Mexico, wamewaambia kwamba hawawezi kuwasaidia kwa sababu ni wengi sana.
Msemaji wa umoja wa mataifa Stephane Dujarric amesema kwamba ni muhimu kwamba mamlaka wanastahili kutoa kifadhi kwa wahamiaji wanaoomba, kwa haraka sana.
Maelfu ya wahamiaji kutoka Amerika ya kati na Haiti, wanakokimbia umaskini na machafuko, wamewasili Mexico wakiwa na matumaini ya kuingia Marekani.