Afisa huyo, Loic Travers, amesema mtu aliyewashambulia polisi hao aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa mwengine wa polisi
Travers amesema mshambuliaji huyo inaaminika kuwa alikuwa ni mfanyakazi katika ofisi hiyo ya makao makuu, lakini hilo linasubiriwa kuthibitishwa.
Travers amesema shambulio hilo linaelekea kuwa lilianza katika ofisi moja na kuendelea kutokea katika maeneo mengine lenye uwanja mkubwa.
Meya Anne Hidalgo amethibitisha “watu kadhaa” kuwa wameuawa.
Hakuna tamko lolote lililotolewa juu ya sababu iliyopelekea shambulio hilo, lililotokea katikati ya Jiji la Paris karibu na Kanisa la Notre-Dame.
Travers amesema, hata hivyo, mshukiwa huyo aliyefanya shambulizi hilo hajawahi kuleta tatizo lolote katika eneo hilo la kazi.