Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 06, 2024 Local time: 09:06

Kundi la pili la maafisa wa polisi 200 wa Kenya lawasili Haiti


Waziri mkuu wa Haiti Garry Conille, akipiga picha na maafisa wa polisi wa Kenya kwenye kambi yao mjini Port-au Prince, Juni 26, 2024. Picha ya AP
Waziri mkuu wa Haiti Garry Conille, akipiga picha na maafisa wa polisi wa Kenya kwenye kambi yao mjini Port-au Prince, Juni 26, 2024. Picha ya AP

Kikosi cha pili cha maafisa wa polisi 200 kutoka Kenya kiliwasili nchini Haiti Jumanne kuimarisha ujumbe unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambao unaongozwa na taifa hilo la Afrika Mashariki kupambana ma magenge ya wahalifu katika taifa hilo la Caribbean lenye mzozo.

Maafisa hao wamewasili karibu mwezi mmoja baada ya kikosi cha kwanza cha polisi 200 kutuwa katika mji mkuu wa Port-au-Prince, ambako magenge yanadhibiti angalau asilimia 80 ya mji huo.

Mamlaka zimekataa kutoa maelezo kuhusu majukumu ya maafisa hao wa Kenya, zikitaja sababu za kiusalama, ingawa wanahabari wa shirika la habari la AP waliwaona wakishika doria katika maeneo karibu na uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa, ambao ulifunguliwa tena mwishoni mwa mwezi Mei baada ya ghasia za magenge kulazimisha kuufunga kwa karibu miezi mitatu.

Polisi zaidi wa Kenya wanatarajiwa kuwasili katika wiki na miezi ijayo na watashirikiana na polisi na wanajeshi kutoka Bahamas, Bangladesh, Barbados, Benin, Chad na Jamaica wapatao 2,500.

Watapelekwa huko kwa awamu kwa gharama ya dola milioni 600 kwa mwaka, kulingana na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG