Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:26

Kiwango cha wawekezaji wa nje kimeshuka Afrika


Viongozi wa nchi za Afrika walipohudhuria mkutano wa ECOWAS huko Abuja, Nigeria on Februari 24, 2024. Picha na Kola Sulaimon / AFP)
Viongozi wa nchi za Afrika walipohudhuria mkutano wa ECOWAS huko Abuja, Nigeria on Februari 24, 2024. Picha na Kola Sulaimon / AFP)

Afrika haikuvutia sana uwekezaji wa kigeni mwaka jana na makubaliano ya kifedha yalishuka kwa asilimia 50 mpaka dola bilioni 64, kwa mujibu wa ripoti mpya.

Ripoti ya World Investment iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo imesema uwekezaji wa kigeni unatokana na kupungua kwa kasi ya uchumi ulimwenguni na kuongezeka kwa mivutano ya kisiasa kijiografia.

Katika bara hilo, nchi za Afrika ya Kati zimerekodi kushuka kwa idadi kubwa sana, asilimia 17, na Afrika Magharibi imerekodi kiwango cha chini sana mpaka asilimia moja.

Bruce Nsereko-Lule ni mshirika mkuu katika Seedstars Africa Ventures, kampuni ya ubia ya mitaji ambayo inawekezaji katika makampuni yenye ukuaji wa juu.

Anasema hali ya uchumi katika mataifa ya Magharibi imechangia kupunguza kwa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni barani Afrika.
“Tumeona viwango vya juu mno vya riba katika uchumi wa mataifa ya Magharibi” alisema Nsereko-Lule.

“Huku kushuka kwa thamani ya sarafu, tumeona hii kwa kiasi imesukumwa na kigezo hicho hicho. Uwekezaji katika masoko haya ya maendeleo, masoko yanayoibukia yamekuwa hayavutii sana wakati makampuni yanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuwa na uzalishaji mzuri ambao utafanya kuwepo na hali nzuri kwa wawekezaji wa Magharibi,” aliongeza.

Viongozi wa nchi za Afrika wakiwa katika mkutano wa nchi za SADC huko Pretoria, October 5, 2021.
Viongozi wa nchi za Afrika wakiwa katika mkutano wa nchi za SADC huko Pretoria, October 5, 2021.

Watafiti wanasema kwamba ukosefu wa mtiririko wa fedha kwa Afrika na nchi nyingine umeathiri maendeleo endelevu, huku ufadhili mpya ukishi kwa asilimia kumi ulimwenguni. Ukosefu wa ufadhili kwa program za maendeleo utaziathiri nchi kufanikisha ajenda ya 2030, ambayo inahusu ukuaji wa uchumi, ujumuishaji wa kijamii na hifadhi ya mazingira.

Kupungua kwa uwekezaji wa kigeni kunalaumiwa kwa sera za ulinzi za serikali ya kiafrika na marekebisho ya kikanda, ambayo wachunguzi wanasema yanavuruga uchumi wa dunia, yanavunja mitandao ya biashara, na mifumo ya udhibiti wa mazingira na usambazaji wa kiamtaifa.

Baadhi ya hatua za serikali zimedhoofisha uthabiti na kutabiri kwa mtiririko wa uwekezaji wa kimataifa, na kuleta vikwazo na kutenga fursa.

Samuel Nyandemo, mhadhiri wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Nairobi, anasema tabia ya baadhi ya serikali za kiafrika inawakimbiza wawekezaji.

“Kuna rushwa, kuna urasimu katika uwekezaji, kuna urasimu kila mahali na halafu kuna viwango vya chini vya faida kutokana na uwekezaji ambavyo havipo.” Nyandemo.

Kuanguka kwa uwekezaji wa moja kwa moja barani Afrika kunalaumiwa na ukosefu wa usalama katika baadhi ya nchi za kiafrika, kudhoofika kwa sarafu ya ndani, mazingira mabaya ya kibiashara, rushwa na ukosefu wa uhakika wa kisiasa.

Wafanyakazi wakiunganisha bajaji ya umeme katika kiwanda kilichopo Khartoum April 19, 2022. Picha na ASHRAF SHAZLY / AFP.
Wafanyakazi wakiunganisha bajaji ya umeme katika kiwanda kilichopo Khartoum April 19, 2022. Picha na ASHRAF SHAZLY / AFP.

Hata hivyo, Afrika imepokea uwekezaji katika kuongezeka kwa mgao wa miradi mikubwa ya kuhifadhi mazingira yenye kugharimu dola bilioni 5, uzalishaji umeme wa upepo na nishati ya jua unaogharimu takriban dola bilioni 10, na Morocco, taifa la Afrika Kaskazini limepatiwa dola bilioni 6.4 ili kuzalishaji betri za magari ya umeme.

Nyandemo anasema Afrika inahitaji kuweka mazingira ambayo wawekezaji watajihisi wako salama na biashara zao.

“Wanahitaji kuwa na imani ya uwekezaji, kuunda mazingira mazuri kwa uwekezaji mkubwa wa kiuchumi na kuwawezesha wawekezaji kuvuna faida kwa njia sahihi bila ya taratibu za kirasimu na kupunguza kodi. Kuweka mfumo wa ushuru ambao ni muafaka kwa uwekezaji,” aliongeza.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inabashiri kwamba licha ya changamoto zilizopo, hali ya kifedha barani AFrika ilitarajiwa kuboreka. Serikali zinaweza kuzungumzia uwekezaji wa chini kwa kuweka mazingira ya biashara ya uwazi na yaliyo rahisi.


Forum

XS
SM
MD
LG