Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 07, 2024 Local time: 23:47

Wawekezaji Afrika Kusini wanataka makubaliano kati ya ANC na DA


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 2, 2024.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akizungumza wakati wa kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 2, 2024.

Randi ya Afrika Kusini imeimarika kwa kiasi mapema leo Jumatatu, huku wachambuzi wakisema wanatarajia kwamba mazungumzo ya kisiasa wiki hii, kuunda serikali yatachochea zaidi thamani ya sarafu hiyo.

Hii ni baada ya chama tawala cha African National Congress ANC kushindwa kupata idadi ya viti vya bunge vinavyohitajika katika utawala wake wa miaka 30.

Randi inabadilishwa kwa kiwango cha 18.73 dhidi ya dola moja ya Marekani, ikiwa imeimarika kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na ilivyokuwa Ijumaa wiki iliyopita.

Chama cha ANC kilipata asilimia 40.2 ya kura, ikiwa ni matokeo mabaya zaidi kuwahi kurekodiwa na chama hicho, na kitalazimika kufanya mazungumo na vyama vingine ili kuunda serikali.

Wawekezaji wana wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa ANC kuhusisha vyama kama EFF cha Julius Malema au uMkhonto we Sizwe cha rais wa zamani Jacob Zuma, na wangependelea ANC kifanye mazungumzo na Democratic Alliance chenye sera za kibiashara.

Forum

XS
SM
MD
LG