Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:03

Kiongozi wa Tigray amtaka Waziri Mkuu wa Ethiopia kuondoa majeshi


Wakimbizi wa Ethiopia wakipanga mstari kuchukuwa chakula katika kambi ya wakimbizi ya Um Rakuba inayo wahifadhi wakimbizi wanaokimbia mapigano huko Jimbo la Tigray, ilioko mpakani kati ya Ethiopia na Sudan, Nov. 28, 2020.
Wakimbizi wa Ethiopia wakipanga mstari kuchukuwa chakula katika kambi ya wakimbizi ya Um Rakuba inayo wahifadhi wakimbizi wanaokimbia mapigano huko Jimbo la Tigray, ilioko mpakani kati ya Ethiopia na Sudan, Nov. 28, 2020.

Kiongozi wa jimbo la kaskazini la Ethiopia linaloshuhudia mapigano la Tigray Debretsion Gebremichael amemwambia Waziri Mkuu Abiy Ahmed aache ukorofi na aondoe wanajeshi wake mara moja.

Amemtaka Abiy kuondoa wanajeshi hao katika jimbo hilo ambalo Gebremichael anadai linaendelea kushuhudia mapigano makali licha ya serikali kutangaza ushindi siku mbili zilizopita.

Kupitia mahojiano kwa njia ya simu na shirika la habari la Reuters mapema Jumatatu, kiongozi huyo wa chama cha Tigray People’s Liberation Army, TPLF, amesema kuwa bado yuko kwenye mji mkuu wa jimbo hilo wa Mekelle, licha ya serikali kudai kuuteka Jumamosi.

Ameongeza kusema kuwa kinyume na madai ya Abiy kuwa wameshinda, mapigano yanaendelea na kwamba ushindi utakuwa wao.

Gebremichael amesema pia baadhi ya wanajeshi wa Eritrea wanaosaidiana na wanajeshi wa serikali wameshikiliwa na wapiganaji wake.

Wakati huo huo, Abiy amekiambia kikao maalum cha Bunge la Ethiopia mapema leo kuwa hakuna raia hata mmoja alieuwawa kwenye mashambulio hayo yaliyoanza Novemba 4 dhidi ya vikosi vya TPLF.

XS
SM
MD
LG