Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:06

Wanajeshi wa Ethiopia wameanza kushambulia mji wa Mekelle


Amlaku Demeke,mmoja wa waathiriwa wa mapigano nchini Ethiopia.
Amlaku Demeke,mmoja wa waathiriwa wa mapigano nchini Ethiopia.

Viongozi wa serikali ya jimbo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopia, wamenukuliwa wakisema kwama wanajeshi wa serikali kuu, inayoongozwa na Waziri mkuu Abiy Ahmed, Jumamosi walianza mashambulizi ya kuuteka na kuudhibiti mji mkuu wa jimbo hilo Mekelle.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba kiongozi wa chama kinanachotwala katika jimbo hilo, TPLF, Debretsion GebreMichael, alituma ujumbe wa Twitter ulioeleza kwamba mji wa Mekele ulikuwa unakabiliwa na mashambulizi makali kutoka kwa wanajeshi wa serikali kuu.

Shirika la habari la Ufaransa AFP pia linaripoti kwamba wafanyakazi wa misaada walishuhudia mashambulizi makali yaliyoulenga mji huo.

Hata hivyo, msemaji wa afisi ya waziri mkuu, Billene Seyum, amenukuliwa akisema kwamba mashambulizi hayo hayatalenga makazi ya raia wa kawaida, na kuongeza kuwa serikali inalipa suala la usalama wa wananchi umuhimu mkubwa.

Utawala wa Abiy, ulikuwa umewapatia wapiganaji wa TPLF hadi Jumatano wiki hii kujisalimisha.

Haya yalijiri huku Umoja wa Mataifa ukisema kwamba Sudan inahitaji masaada wa takriban dola za Marekani 150 kwa minajiri ya kugharamia kambi kubwa la wahamiaji wanaoendelea kuvuka mpaka kutoka nchi jirani ya Ethiopia, kufuatia mapigano hayo.

Akizungumza Jumamosi kwenye kambi ya wakimbizi ya Um Raquba, iliyo umbali wa kilomita 80 kutoka kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili, Kamishna mkuu wa Shirika la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grande, alitoa wito kwa wafadhili wa kimataifa kusaidia kuchanga kiasi hicho cha pesa haraka iwezekanavyo ili kuokoa maisha ya maelfu ya watu.

Mapigano kati ya wanajeshi wa serikali kuu ya Ethiopia na wapiganaji wa chama kinachotawala katika jimbo la Tigray cha TPLF yalianza tarehe 4 mwezi Novemaba na tayari Sudan ni mwenyeji wa zaidi ya Waethiopia 43,000 waliokimbia vita hivyo.

XS
SM
MD
LG