Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 12:55

Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso amfukuza waziri mkuu na kuivunja serikali


Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kepteni Ibrahim Traore. Picha ya Reuters
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kepteni Ibrahim Traore. Picha ya Reuters

Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Ijumaa alimfuta kazi waziri mkuu na kuvunja serikali, kulingana na amri ya rais iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.

Waziri mkuu aliyefukuzwa aliongoza serikali tatu mfululizo, akinusurika kila yanapofanyika mabadiliko ya baraza la mawaziri.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kumfuta kazi Apollinaire Joachim Kyelem, ambaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu mwezi Oktoba 2022 baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomuweka madarakani kepteni Ibrahim Traore.

Nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilitumbukia katika ukosefu wa usalama kufuatia mapinduzi ya Januari 2022 ambapo Luteni Kanali Paul Henri Sandaogo Damiba alichukua madaraka.

Forum

XS
SM
MD
LG