Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:37

Kiongozi wa Al-Qaida tawi la Yemen auwawa kupitia shambulizi


Kiongozi wa al-Qaida tawi la Yemen, Khalid al Batarfi , aliyeuwawa
Kiongozi wa al-Qaida tawi la Yemen, Khalid al Batarfi , aliyeuwawa

Tawi la Al-Qaida nchini  Yemen Jumatatu limetangaza kifo cha  kiongozi wake Khalid al Batarfi  kilichotokea Jumapili.

Hata hivyo video iliyotolewa na kundi hilo haikutoa maelezo yoyote kuhusu kifo chake, ingawa imemuonyesha akiwa amefunikwa na kitambaa kwa ajili ya mazishi, pamoja na bendera ya kundi hilo la wanamgambo, kwa mujibu wa taarifa za kundi la kiintelijenisia la SITE.

Marekani iliahidi tuzo ya dola milioni 5 kwa atakayetoa taarifa kuhusu mahali alipo al-Batafri, ambaye amekuwa kiongozi wa al-Qaida kwenye Peninsula ya Kiarabu, AQAP, tangu Februari 2020. Kufuatia kifo hicho, kundi lilo limemtangaza Saad bin Atef al-Awlaki, ambaye pia Marekani imeahidi kutoa dola milioni 6, kwa atakayetoa taarifa kuhusu mahali alipo, kujaza nafasi ya al-Batafri.

Tawi la AQAP, kwa muda mrefu limechukuliwa kuwa tawi hatari zaidi la al-Qaida, na limelaumiwa kufanya mashambulizi mabaya kama lile la 2015, dhidi ya ofisi za gazeti la vichekesho la Ufaransa la Charlie Hebdo. Kiongozi al-Batafri, Qassim al-Rimi aliuawa na droni ya Marekani kama majibu ya shambulizi la 2019, dhidi ya kituo cha jeshi la Maji la Marekani jimboni Florida.

Forum

XS
SM
MD
LG