Mkuu wa majeshi ya Pakistan yuko mjini Washington wiki hii akitafuta msaada wa Marekani dhidi ya kile Islamabad inadai kuwa ni maeneo ya magaidi katika nchi jirani ya Afghanistan.
Jenerali Asim Munir anajaribu kuwashawishi maafisa wa usalama na ulinzi wa Marekani, kwamba makundi ya wanamgambo kama vile Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP) na Islamic State’s Khorasan (IS-K) yanaweka tishio sio tu kwa Pakistan bali pia kwa Marekani na usalama wa ulimwengu, wataalamu wanasema.
Siku ya Jumatano, Munir alikutana na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin na walijadili “maendeleo ya hivi karibuni ya usalama wa kikanda na maeneo ya uwezekano wa ushirikiano wa ulinzi wa nchi mbili”, kulingana na taarifa fupi kutoka Pentagon.
Licha ya kuondolewa kwa wanajeshi wake kutoka Afghanistan zaidi ya miaka miwili iliyopita, Marekani imebakiza kile ambacho maafisa wa Marekani wanakiita kuwa ni uwezo wa juu katika eneo hilo, uwezo wa kushambulia malengo katika majibu ya vitisho vya usalama.
Hapo Julai 2022, shambulio la ndege isiyo na rubani la Marekani lilimuua Ayman al-Zawahiri mkuu wa zamani wa al-Qaida mjini Kabul.
Forum