Nchi saba za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zilianzisha kikosi cha kijeshi cha EACRF mwezi Aprili mwaka jana ili kujaribu kumaliza umwagikaji wa damu unaohusishwa na miongo kadhaa ya shughuli za wanamgambo mashariki mwa Kongo.
Mustakabali wa kikosi hicho ulikuwa haujulikani tangu muda wake ulipomalizika mwezi Machi, na viongozi wa EAC walikuwa wametoa maoni tofauti kuhusu jinsi kinavyopaswa kufanya kazi.
Mashaka juu ya ufanisi wake yaliongezeka mwezi Aprili baada ya mkuu wa kikosi hicho, Meja Jenerali Jeff Nyagah, kusema kuwa amejiuzulu kutokana na vikwazo na vitisho kwa usalama wake.
Jumatano, msemaji wa EAC alithibitisha ripoti kwamba mamlaka ya kikosi hicho yameongezwa hadi Septemba wakati wa mkutano wa kilele nchini Burundi.
Waziri wa Ulinzi wa Kongo Jean-Pierre Bemba pia alithibitisha ripoti hizo.
Rais Felix Tshisekedi amekuwa akikosoa EACRF waziwazi, akishutumu kikosi hicho kwa kutokuwa na nguzu vya kutosha na kushindwa kuwadhibiti waasi wa M23, ambao walianzisha mashambulizi mashariki mwa nchi mwaka jana.
Awali Tshisekedi alikuwa amekubali kuongeza muda wa EACRF hadi Juni.
Forum