Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:10

Kerry awapongeza wananchi Kenya kwa kujitokeza kupiga kura


Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry na Waziri Mkuu wa Senegal Aminata Touré, wakiwa katika shule ya msingi ya Westlands Nairobi.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry na Waziri Mkuu wa Senegal Aminata Touré, wakiwa katika shule ya msingi ya Westlands Nairobi.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amesema Jumatano mistari mirefu ambayo ameiona katika vituo vya kupiga kura ni alama ya ahadi ya wananchi kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.

Kwa mujibu wa VOA Kerry na aliyekuwa waziri mkuu wa Senegal Aminata Toure Viongozi pacha wa Kituo cha Carter Center cha usimamizi wa uchaguzi walitembea shule ya Sekondari ya Jamhuri Jijini Nairobi.

“Ni mapema sana kwetu kutoa majumuisho ya aina yoyote kuhusu uchaguzi, kwa hiyo hatutofanya hivyo, lakini kutokana na yale yaliotokea huko nyuma na kufuatia hatari za siku za usoni, huu ni uchaguzi muhimu sana na wananchi wa Kenya bila shaka wanauchukulia uchaguzi huu kwa makini sana,” amesema Kerry.
Tume ya uchaguzi Kenya inatumia mifumo ya biometric katika kutambua wapiga kura na pia upeperushaji wa kura kielektroniki katika zeozi zima la uchaguzi.

Kura inatizamwa kama ni kipimo kikubwa kwa tume katika kufanikisha uchaguzi mwaka huu baada ya teknolojia ya kupiga kura kufeli wakati wa uchaguzi wa mwisho wa mwaka 2013 na kuzua tuhuma za wizi wa kura.

Pia wito wa amani katika matokeo ya uchaguzi umetolewa Jumatatu na rais mstaafu wa Marekani Barack Obama, mtoto wa mzazi ambaye ni mwananchi wa Kenya.

Obama amewahimiza wapiga kura katika nchi ya wazee wake kukataa uvunjifu wa amani na uchochezi; kuheshimu uamuzi wa wananchi; na kuvitaka vyombo vya ulinzi kufuata weledi katika kazi yao na kutopendelea upande wowote; na kushirikiana bila ya kujali matokeo ya uchaguzi.

Mshindi wa uchaguzi wa rais lazima apate asilimia 50 za kura zote, na asilimia 25 au zaidi ya kura angalau katika kaunti 25 kati ya kaunti 47 nchini Kenya. Ikiwa wote hawajapata idadi hiyo ya kura, itawalazimu kuingia kwenye raundi ya pili ya uchaguzi.

XS
SM
MD
LG