Amiri Jeshi Mkuu wa Kenya akiwa amevalia magwanda ya kivita, alikutana na majeshi ya Kenya na kuwashukuru kwa kujitoa mhanga na kulitumikia taifa lao.
Hii ni ziara ya kwanza ya Rais Kenyatta kutembelea Somalia katika hali ya kuongeza morali kwa majeshi ya Kenya.
Rais tayari ameshatembelea makao makuu ya Somalia, Mogadishu siku za nyuma katika shughuli za kiserikali.
Rais amewaambia wanajeshi kuwa taifa la Kenya litakuwa siku zote ina deni kwa wanajeshi hao ambao wamekuwa mstari wa mbele kutokomeza vitisho vya al-Shabaab.
“Kuwepo kwenu Somalia kumesaidia watu wengi, na kwa hilo Wakenya wataendelea kuwa na deni la kulipa fadhila kwenu wapiganaji wetu. Kuwepo kwenu Somalia kwa kiwango kikubwa kumewaondoshea watu wetu hofu ya al-Shabaab,” Rais Kenyatta amesema.
Rais amesema; “ Tumeweza kuifufua sekta ya utalii kwa sababu ya ujasiri wenu wa kuifanya nchi yetu iwe na amani.”
Kambi ya Kijeshi ya Dhobley ni makao makuu ya AMISOM, Kituo cha mawasiliano na kumbukumbu muhimu za Umoja wa Mataifa (UN).