Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 23:09

Kenya yasema imewakabidhi wakimbizi wanne raia wa Uturuki baada ya kukubali ombi la nchi yao


Rais wa Kenya William Ruto akizungumza na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kwenye Umoja wa Mataifa Septemba 25, 2024 huko New York.
Rais wa Kenya William Ruto akizungumza na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kwenye Umoja wa Mataifa Septemba 25, 2024 huko New York.

Kenya ilisema Jumatatu imewakabidhi wakimbizi wanne raia wa Uturuki baada ya kukubali ombi la Ankara la  kutawaka warejeshwe nchini kwao

Hilo limefanyika licha ya shirika la Amnesty International kuelezea wasiwasi kuwa wanaweza kukabiliwa na mateso nyumbani ikiwa watafukuzwa nchini.


Ilikubali ombi la kuwafukuza kwa sababu ya uhusiano wenye nguvu kati ya nchi hizo mbili, taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora ilisema, na kuongeza kuwa ilipata uhakikisho kwamba watu hao wanne watatendewa kwa heshima kwa kuzingatia sheria za kitaifa na kimataifa.


Amnesty ilisema Jumamosi kwamba ikiwa watafukuzwa wanaweza kukabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ambao ilisisitiza wasiwasi unaoongezeka kuhusu usalama wa wakimbizi wote na wanaotafuta hifadhi nchini Kenya.

Kenya ilisema imejitolea kuwalinda wakimbizi wapatao 780,000 inaowahifadhi, wengi wao wakiwa wanatokea nchini Somalia.

Forum

XS
SM
MD
LG