Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 17:32

Kenya yakabiliwa na uhaba wa mafuta


Wateja wakisubiri katika foleni ya ununuzi wa mafuta katika kituo cha Petroli cha Shell Nairobi, Kenya, Aprili 4, 2022. (Photo by Simon MAINA / AFP)
Wateja wakisubiri katika foleni ya ununuzi wa mafuta katika kituo cha Petroli cha Shell Nairobi, Kenya, Aprili 4, 2022. (Photo by Simon MAINA / AFP)

Uhaba mkubwa wa mafuta Kenya unazidi kuliumiza taifa hilo huku miji mikubwa ikiripoti misururu mirefu katika vituo vya kuuza mafuta ambavyo vina bidhaa hiyo.

Kuna sababu zinazokinzana kuhusu kwa nini uhaba wa mafuta umejitokeza sasa.

Rais Uhuru Kenyatta amesema ni kutokana na mzozo wa kidunia uliyosababishwa na Russia kuivamia Ukraine.

Kampuni ya taifa ya mafuta, Kenya Pipeline, imesema kuwa kuna akiba ya kutosha ya mafuta na mdhibiti EPRA imeionya kampuni yoyote inayohodhi mafuta hayo kupunguza udhibiti.

Wachambuzi wanasema ruzuku iliyocheleweshwa iliyoahidiwa na serikali kwa wauzaji mafuta ili kuwapa afueni wanunuzi kutokana na athari za mzozo wa dunia inasababisha uhaba huo.

XS
SM
MD
LG