Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 23:58

Kenya yaanza zoezi la kuhamisha ndovu kutokana na msongamano


Ndovu wakiwasili kwenye makao mapya ya mbuga ya kitaifa ya Aberdare kati kati mwa Kenya, Oct. 14, 2024.
Ndovu wakiwasili kwenye makao mapya ya mbuga ya kitaifa ya Aberdare kati kati mwa Kenya, Oct. 14, 2024.

Kenya imeanza kuhamisha ndovu kutoka kwenye mbuga ya kitaifa ya wanyamapori ya Mwea,  iliyopo mashariki mwa Nairobi baada ya idadi yao kuongezeka kutoka 50 hadi 150, na kwa hivyo kulemea mbuga hiyo yenye ukubwa wa kilomita 42 mraba.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, mkuu wa Idara ya kitaifa ya wanyamapori Erustus Kanga, amesema kuwa idadi kubwa ya ndovu kwenye mbuga ya Mwea ni ishara ya utunzaji bora wa wanyama hao ndani ya miongo mitatu iliyopita. “Hii ni ishara kuwa uwindaji haramu umeshuka, na kwamba ndovu wanashamiri,” Kanga ameongeza kusema.

Wataalam walianza kuhamisha ndovu 50 wiki iliopita hadi kwenye mbuga ya kitaifa ya Aberdare yenye ukubwa wa kilomita 780 mraba, na kufikia Jumatatu, tayari ndovu 44 walikuwa wamehamishwa. Wengine 6 wamepangwa kuhamishwa Jumanne. Waziri wa Utalii Rebecca Miano alikuwa miongoni mwa watu walioshuhudia uhamishaji wa ndovu watano Jumatatu. Shughuli yenyewe ilianza alfajiri ikihusisha zaidi ya wataalam 100, wakiwa na vifaa maalum kama magari na ndege.

Forum

XS
SM
MD
LG