Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 05:29

Wabunge wamshinikiza Kabudi kuwepo katiba mpya Tanzania


Prof Kabudi
Prof Kabudi

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Kabudi Jumamosi amefika mbele ya Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge na kushinikizwa kutoa maelezo kuhusu mchakato wa Katiba mpya ulipofikia.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari Dodoma mkutano huo ni wa kwanza tangu ashike wadhifa wa uwaziri baada ya Dk Harrison Mwakyembe kuhamishiwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Wabunge wa CCM walimbana Profesa Kabudi kuhusu Katiba Mpya. Katika mkutano huo wameibua suala kuhusu mchakato wa katiba mpya.

Profesa Kabudi baada ya kufika mbele ya Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, akiwa katika nafasi ya uwaziri alisema hajakutana na viongozi wake kuzungumzia suala la Katiba Mpya, akiwemo Waziri Mkuu.

Lakini alikiri kuwa anajua mambo mengine kuhusu mchakato huo ambao wakati wa maandalizi yake, alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Wabunge wa CCM walikuwa wa kwanza kuibua hoja hiyo jana wakisema Katiba Mpya ni sehemu ya ilani ya uchaguzi ya chama chao.

Mbunge wa Bahi (CCM), Omari Badwel alimtaka waziri huyo aseme ni lini hasa mchakato huo utaendelea na Watanzania watarajie kuipata lini Katiba hiyo.

Mbunge huyo aliuliza wapi mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 yameorodheshwa na ni kifungu gani kitakachotumika kwa ajili ya kusaidia mchakato wa katiba hiyo.

“Hata humu sijaona kama kuna fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya, najiuliza ina maana si kipaumbele au mmesahau kuwa hata ilani ya uchaguzi ya CCM imetaja suala hilo?” alidadisi Badwel.

Mbunge wa Malindi (CUF), Ali Saleh amesitiza kwamba suala hilo kwa kuwa ni muhimu mbona linachukua muda mrefu kukamilika.

Mbunge huyo ambaye alikuwa miongoni mwa wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alilalamika kuwa suala la Katiba Mpya limezimwa.

Ameinasihi serikali kusoma alama za nyakati, kwani huu ndiyo wakati mwafaka.

XS
SM
MD
LG