Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:43

'Kashfa ya madini isiishie kuwavua madaraka wachache'


Freeman Mbowe
Freeman Mbowe

Chama cha upinzani nchini Tanzania kimesema kuwa wale wote waliohusika kusaini na kuingia mikataba iliyochangia taifa kuibiwa rasilimali zake, wawajibishwe, badala ya kuishia kuwavua madaraka watu wachache.

Vyanzo vya habari nchini Tanzania vimesema aidha upinzani umesema kuwa utafiti uliofanywa na repoti yake kuwasilishwa katikati ya wiki na Kamati ya Profesa Abdulkarim Mruma, si ya kwanza.

Wamedai kuwa mambo yaliyogusiwa katika repoti hiyo yaliwahi kuelezwa pia na Kamati ya Jaji Mark Bomani na pia mashirika ya nje, yote yakisisitiza kuwa mikataba ya madini nchini hainufaishi taifa.

Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe aliyasema hayo Jumamosi Dodoma na kuongeza kuwa suala la kujenga mtambo wa kuchenjua makinikia ya mchanga wenye madini ni muhimu kwa sasa na kwamba hilo linawezekana.

Alisema hata wabunge wa kambi ya upinzani, kwa muda wamekuwa wakilalamikia mikataba iliyoingiwa baina ya Serikali na wawekezaji katika madini kuwa haikuwa na maslahi wala faida kwa watanzania.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema chama chake kinaamini tatizo halipo kwa wawekezaji katika kusafirisha mchanga, bali ni mikataba iliosainiwa.

Amesema ilikuwa vyema kabla kiongozi wa nchi hajazuia makontena, mikataba yake ingeletwa bungeni hata kwa hati ya dharura ikabadilishwa, kama ilivyofanyika wakati iliposainiwa, ambapo kwa siku moja mikataba miwili ilisainiwa.

Amesema mikataba hiyo ndiyo inayoruhusu mwekezaji atozwe dola 200,000 (Sh milioni 420) kwenye mradi wa dhahabu, badala ya kutozwa kwa kutumia asilimia 0.14 ya mapato yatokanayo na madini yanayochimbwa na Chadema inaona suluhisho ni kuifanyia marekebisho.

XS
SM
MD
LG