Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 02:39

Kamanda wa zamani wa LRA nchini Uganda apatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu


Waasi wa LRA
Waasi wa LRA

Kamanda wa zamani wa kundi la waasi la Lord Resistance Army (LRA) alipatikana na hatia kwa makosa kadhaa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu katika hatua muhimu ya utendaji wa haki kwa watu wengi nchini Uganda walioteseka kwa miongo kadhaa kutokana na uasi wake wa kikatili.

Uamuzi huo uliosubiriwa kwa muda mrefu katika kesi ya Thomas Kwoyelo ulitolewa Jumanne na jopo la Mahakama Kuu katika mji wa kaskazini wa Gulu, ambako LRA iliwahi kuendesha uasi wake.

Ilikuwa kesi ya kwanza ya ukatili kusikilizwa chini ya kitengo maalum cha Mahakama Kuu ambacho kinafuatilia uhalifu wa kimataifa.

Haikufahamika wazi ni lini atahukumiwa.

Kwoyelo, ambaye kesi yake ilianza mwaka 2019, amekuwa akishikiliwa tangu mwaka 2009, huku mamlaka ya Uganda ikijaribu kutafuta jinsi ya kutekeleza haki kwa njia ya haki na ya kuaminika.

Shirika la haki za binadamu Human Rights Watch liliielezea kesi yake kama “fursa nadra ya kuwatendea haki waathirika wa vita vya miongo miwili” kati ya wanajeshi wa Uganda na LRA.

Forum

XS
SM
MD
LG