Tuhuma hizo ni pamoja na mauaji, manyanyaso ya kingono, kuwateka watoto, wizi wa ngawira, katika uamuzi kwenye mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa.
Ongwen, aliyewahi kuwa kamanda katika Jeshi la Lord's Resistance, anakabiliwa na mashtaka 70 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Pia anaweza kupewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani.
Hata hivyo majaji hawata zungumzia hukumu siku ya Alhamisi.
Jaji anayesimamia kesi hiyo Bertram Schmitt alisema ushahidi katika kesi ya Ongwen ulionyesha kuwa uhalifu wa kijinsia ulikuwa wa kimfumo na kitaasisi chini ya amri yake na katika sheria kwanza walimhukumu kwa uhalifu wa ujauzito wa kulazimisha.