Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 23:30

Jumuiya ya Afrika Mashariki yaridhia hatua ya EU kuiondolea vikwazo Burundi


Rais wa Burundi Evariste Ndayshimiye (Katikati).
Rais wa Burundi Evariste Ndayshimiye (Katikati).

Jumuiya ya Afrika Mashariki imefurahishwa na hatua ya Umoja wa Ulaya kuiondolea Burundi vikwazo vya kiuchumi ilivyokuwa imewekewa karibu miaka sita iliyopita.

Katibu mkuu wa jumuiya hiyo, Peter Mathuki, amesema kwamba hatua hiyo ya umoja wa ulaya inatarajiwa kufufua ukuaji nchini Burundi na kuchochea ushirikiano wa maendeleo katika jumuiya ya Afrika mashariki.

Umoja wa ulaya unafadhili miradi ya biashara, utawala, amani, usalama, kuhifadhi mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa, katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki.

Mathuki amesema kwamba miradi hiyo itaimarika zaidi kufuatia hatua hiyo ya kuiondolea vikwazo serikali ya Burundi.

Burundi iliwekewa vikwazo mnamo mwaka 2016 baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu madarakani, hatua iliyosabisha maandamano makubwa na kupelekea vifo vya watu.

XS
SM
MD
LG