Sehemu ya 1: Juhudi za amani na maendeleo DRC . |
Katika miaka 50 ya uhuru, Jamhuri ya Kidemokrasia yan Kongo imeshuhudia, ghasia miaka ya kwanza kunyakua uhuru ikifuatiwa na miaka 40 ya utawala wa kimabavu, ulondolewa madarakani na mapinduzi, na kufuatiwa mapigano yaiyohusisha mataifa jirani. Hii leo juhudi za amani zinatekelezwa hasa huko mashariki ya nchi wakati wa serikali ya rais Joseph Kabila ikijaribu kuleta maendeleo kwa kuzingatia kujenga miundo mbinu na kukuza sekta ya madini.
Kitu cha kwanza alipochukua madaraka baada ya kuuliwa kwa babake, Joseph Kabila alifikia makubaliano Febuari 2001 na Rwanda na Uganda na kupelekea kuondolewa majeshi yote ya kigeni na kuwasili majeshi ya amani ya UM, MONUC April 2001.
Licha ya kupatikana amani hiyo ugomvi ulizuka tena hapo januari 2002 kwa mapigano ya kikabila huko kaskazini mashariki na hapo Uganda na Rwanda zikasitisha kuondoa majeshi yao na badala yake kuongeza majeshi zaidi. Na baada ya mazungumzo ya amani Kabila akalazimika kugawanya madaraka na viongozi wa makundi ya zamani ya uwasi, Jean pierre bemba, Mbusa Nyamwisi na Azarus Ruberwa ambao walikua makamu rais wa serikali ya mpito.
Katiba mpya iliidhinishwa na wananchi na uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia tangu uhuru ulifanyika July 30 2006. Josep Kabila alijipatia asili mia 45 za kura katika duru ya kwanza dhidi ya mpinzani wake mkuu Bemba aliyejipatia asili mia 20, na ugomvi ulizuka kutokana na mabishano juu ya matokeo hayo na kupelekea mapambano katika mji mkuu wa Kinshasa hapo Augusti 2006, watu 16 waliuwawa. Duru ya pili ya uchaguzi ilifanyika na Kabila kupata ushindi wa asili mia 70 za kura. Serikali ya mpito ilivunjwa Disemba 6 2006 na Kabila kuapishwa rais.