Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 03:32

Miaka 50 ya Uhuru wa DRC


Patrice Lumumba, waziri mkuu wa Congo akitia saini tangazo la uhuru mjini Leopodville, Congo. Kulia kwake ni waziri mkuu wa zamani wa Ubelgiji Gaston Eyskens, aliyretia saini kwa niaba ya Ubelgiji. Ubelgiji iliitawala Congo kwa miaka 70.
Patrice Lumumba, waziri mkuu wa Congo akitia saini tangazo la uhuru mjini Leopodville, Congo. Kulia kwake ni waziri mkuu wa zamani wa Ubelgiji Gaston Eyskens, aliyretia saini kwa niaba ya Ubelgiji. Ubelgiji iliitawala Congo kwa miaka 70.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeadhimisha miaka 50 ya uhuru Juni 30 kwa sherehe kubwa.

Sehemu ya 1:

Kipindi cha vita vya uhuru wa DRC .

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeadhimisha miaka 50 ya uhuru Juni 30 kwa sherehe kubwa ambazo zimehudhuriwa na viongozi kadha kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Mfalme Albert wa pili wa Ubelgiji ambayo ilitawala Congo. Mfalme huyo wa Ubelgiji ni kiongozi wa kwanza kutoka katika ufalme wa nchi hiyo kutembelea Congo katika kipindi cha miaka 25. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon pia ni miongoni mwa wanaohudhuria sherehe hizo.

Viongozi wengine kadha wa Afrika ikiwa ni pamoja na nchi za jirani kama vile Paul Kagame wa Rwanda pia wanahudhuria sherehe za kitaifa katika mji mkuu Kinshasa.

Sherehe hizo zinafanyika huku Congo ikiwa inakabiliwa na changamoto mbali mbali. Ingawaje nchi hiyo ina akiba kubwa ya madini kama vile dhahabu, almasi na shaba, ni moja ya mataifa masikini sana duniani.

Congo bado ina machungu ya historia ngumu, iliyokuwa na utawala wa kikatili wa Mfalme wa zamani wa Ubelgiji Leopold, mauaji ya kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, Patrice Lumumba, utawala wa kidikteta wa Mobutu uliodumu kwa miaka 32, na vita ya hivi karibuni iliyosababisha vifo vya watu wapatao millioni tatu.

Umoja wa Mataifa una walinzi wa amani elfu 20 nchini humo, idadi kubwa kuliko duniani. Hata hivyo, Rais wa DRC Joseph Kabila anataka walinzi hao wa amani waondoke Congo ifikapo mwaka 2011.

Kwenye ukurasa huu unaweza kusikiliza maelezo ya kisiasa, kihistoria, kiuchumi na mustakbala wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

XS
SM
MD
LG